JINA MIZI LA ARSENE WENGER LAWAKUMBA BENCHI ZIMA LA UFUNDI,WOTE WAFUTWA KAZI NAO.
Watu sita wa muda mrefu katika benchi la Ufundi la Arsenal wameondolewa wakimfuata aliuekuwa bosi wao, Mfaransa Arsene Wenger.
Klabu inajiandaa kwa zama mpya kabisa baada ya kuondoka kwa Arsene Wenger aliyedumu kwa miaka 22 na Mkuu wa Idara ya Tiba, Colin Lewin pamoja na makocha wasadizi Neil Banfield, Gerry Peyton, Tony Colbert na Paul Johnson wote wameondolewa.
Wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Wenger ni wachezaji wa zamani wa klabu hiyo, Mikel Arteta ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Pep Guardiola pale Manchester City, Patrick Vieira, ambaye kwa sasa ni kocha wa New York City, Julian Nagelsmann, ambaye kwa sasa anafundisha Hoffenheim anaeongoza mbio.
Inaelezwa kwa sababu za kifedha, klabu imeachana na mpango wa kuwafukuzia Luis Enrique na Massimiliano Allegri.
No comments: