Header Ads

CHELSEA>>MAURICIO POCHETTINO KUVAA VIATU VYA ANTONIO CONTE ,MSIMU UJAO.




Klabu ya Chelsea huenda ikampa ajira kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino, kama Antonio Conte ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu. 

Conte amekuwa akihushwa kuachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu licha ya waajiri wake kutothibitisha taarifa hizo. Huu ni msimu wa pili kwa kocha huyo baada ya kufanya vyema kwa kutwaa taji la EPL miezi 12 iliyopita akiwa na Chelsea. 

Taarifa zinasema kuwa, klabu ya Chelsea hipo mbioni kutafuta kocha atakaeziba nafasi ya Conte, huku makocha kama vile Luis Enrique, Maurizio Sarri, na sasa Pochettino wanatajwa kuziba nafasi hiyo. 



Pochettino alijiunga na Spurs mwaka 2014 mwezi May, huku akifanikiwa kuifanya Tottenham kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA mara 3 mfululizo. 

Wachambuzi wa masula ya soka wanasema kuwa Pochettino ni kocha mzuri kwa Chelsea kwani, ameonesha ubora wake akiwa na Spurs huku akifanikiwa kuleta ushindani na timu zinazotumia gharama kubwa kuunda vikosi vyao . 

Kuna wakati kocha Pochettini alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa, Kocha Pep Guardiola wa Man City, anatumia gharama kubwa kulinunua kombe la EPL na siyo uwezo aliokuwa nao wa kufundisha soka. 

Kauli hiyo ya Pochettino ilikuja baada ya kocha Pep kudai kuwa Spurs imekuwa timu ya mtu mmoja tu, ambaye ni Harry Kane. 

Pochettino ambaye ni raia wa Argentina amebakiwa na miaka mitatu katika mkataba wake wa kuinoa Spurs huku, akiwa na mpango wa kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa klabu hiyo ili kuiongeza bajeti ya usajili kwa msimu ujao. 

Katika msimu huu wa 2017/2018, Conte hajafanikiwa sana kwani ameifanya chelsea kushindwa kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA msimu ujao licha ya kuifikisha fainali ya kombe la FA.

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.