Header Ads

KANE>>KAMA KWELI SALAH NI MFUNGAJI BORA NA MWAKANI ACHUKUWE TENA UFUNGAJI BORA TUONE.

Image result for kane
Straika wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane amempa changamoto mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kuwa kama kweli anataka kutambulika kama mfungaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza basi avunje rekodi aliyoiweka yeye ya kutwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo. 

Kupitia mahojiano yake na vyombo vya habari Kane amesema nivizuri kuwa na ushindani na inavutia kuona kwenye ligi ya Uingereza kunakuwa na wachezaji wawili waliyofanikiwa kufunga mabao 30. 

"Ni vizuri kuwa na ushindani, na inavutia zaidi kuona kwenye ligi ya Uingereza kunakuwa na wachezaji wawili waliyofanikiwa kufunga mabao 30. 

Binafsi yalikuwa ni malengo yangu kuona kipaji changu kinakuwa ukilinganisha na mwaka jana, wakati nilifunga mabao 29 msimu huu nimefikisha 30 kwangu naona vizuri. 

Mo amefanya vizuri mwaka huu, hakika anastahili kupata tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu naangazia zaidi kwenye ushindani wetu mwaka ujao. 

Kila mchezaji anahitaji kuwa na muendelezo mzuri kila msimu na hiyo ndiyo tafsiri ya mchezaji mzuri kuwa bora. Amefanya kitu kizuri na kinashangaza msimu huu na anaonekana kuwa mchezajibora tutaona kama tutaendelea kuwa hivi msimu ujao". 

Licha ya kupoteza tuzo hiyo, Kane mwenye mabao 30, anaamini kuwa amefanya vema zaidi msimu huu baada ya misimu miwili iliyopita kufunga 25 na 29 na kuongoza kuchukua kiatu cha dhahabu mara mbili mfululizo.

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.