IJUWE LISHE BORA KWA MTOTO WAKO,HUSUSANI KWA MTOTO WA MWEZI 1-6 NI MUHIMU KUZINGATIA HAYA.
Kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua.
FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA
Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.
Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti.
Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu.
WAKATI GANI WA KUANZA KUMWANZISHIA MTOTO VYAKULA VINGINE
Mtoto wako akifikisha miezi 6 unaweza kuanza kumpatia vyakula vingine kidogo kidogo ( Kuna ambao kutokana na sababu Fulani daktari huwashauri kuanza mtoto akiwa na miezi 4 hivyo ni vyema ukiwasiliana na daktari wako kwanza). Mtoto akianza kupewa vyakula nje ya maziwa mapema kabla ya miezi 4 ni hatari kwa afya yake maana mfumo wake wa kusaga chakula unakuwa bado haujawa tayari. Unapoanza kumpa vyakula vingine hauachi kumnyonyesha, unyonyeshaji unaendelea hadi miaka miwili na nusu.
Akishafikisha miezi 6 Endelea kunyonyesha na anza kumpa vyakula vyenye madini ya chuma. Mtoto alishwe kwa ratiba inayoeleweka kila siku na katika ratiba hiyo hakikisha angalau mara moja kwa siku muda wake wa kula unakuwa sawa na muda wa familia yote ili muweze kula pamoja. Vyakula vyake viwe vimepondwapondwa kabisa ikiwezekana tumia blender na hakikisha anapata mlo kamili yani matunda, mbogamboga, mbegu, nafaka, nyama na samaki. Inashauriwa kutokuchanganya aina tofauti za nafaka kwenye unga mmoja unapomtengenezea uji, uwe na unga wa mahindi, ulezi,mchele n.k tofauti tofauti. Pika aina moja ya uji kwa wakati unaweza kufanya kwa wiki au vyovyote utakavyopenda.
No comments: