EVAERTON>>ALLARDYCE ATUMIKIA MIEZI 6 PEKE YAKE KATIKA CLABU YA EVERTON NA SASA AFUNGASHIWA VIRAGO VYAKE.
Klabu ya Everton imetangaza kumfuta kazi Kocha wake, Sam Allardyce, kutokana na matokeo yasiyoridhisha msimu huu ulioisha na , tovuti ya klabu hiyo imeeleza.
Baada ya kuitumikia Everton kwa miezi 6, Uamuzi wa kumtimua kocha huyo umekuja baada ya mkutano baina yake na mwenyekiti wa klabu hiyo Farhad Moshiri ambaye ameamua kumfungia vilago Allardyce.
Allardyce mwenye umri wa miaka 63 ameiwezesha Everton kumaliza katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu lakini matokeo hayo yameshindwa kulinda kibarua chake.
Kocha huyo atalipwa kiasi kinachokadiriwa kufikia paundi milioni 6 ikiwa ni malipo ya miezi 12 iliyobaki katika mkataba wake.
Kocha wa zamani wa Watford Marco Silva anatajwa kumrithi Sam Allardyce kwani Everton walimtaka tangu mwaka jana mwezi Novemba wakati mreno huyo akiwa Watford.
Rekodi ya Sam Allardyce Everton.
26 games
10 wins
7 draws
9 losses
38.5% win rate
No comments: