HABARI NJEMA KWA WANA MICHEZO YOUTUBE KUUONYESHA FINAL ZA UEFA.......
Shirika la michezo la BT Sports limeamua kuuonesha mchezo huu bure kabisa, kupitia channel yao ya Youtube, BT Sports wataonesha mechi hii moja kwa moja kutoka mjini Kiev na ni data tu ndizo utatumia.
Katika fainali ya msimu uliopita ya Champions League kati ya Real Madrid vs Juventus BT Sports walivutia jumla ya watazamaji 6.5m dunia nzima na wanaamini safari hii uwepo wa klabu toka Uingereza utaongeza watazamaji.
Katika kutanua wigo wa kuongeza watazamaji, mchezo huu pia utaoneshwa katika application ya BT Sports pamoja na website yao, na yeyote mwenye app hiyo ataweza kuuona mchezo huo moja kwa moja kutoka Kiev.
Peter Oliver ambaye ni mkurugenzi wa BT Sports amekiri kwamba uwepo wa Liverpool katika fainali hii ni fursa kubwa katika biashara ya uoneshaji mpira na wataitumia fursa hiyo kuongeza mashabiki dunia nzima.
No comments: