Header Ads

Ancelotti kumng’oa conte chelsea



Siku za Antonio Conte kuinoa Chelsea zimezidi kupungua kwa kasi baada ya Carlo Ancelotti, kuripotiwa kuwa njiani kujiunga na Napoli. 

Iko hivi, kitendo cha Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis, kukutana na Ancelotti juzi usiku kinamaanisha kuwa Maurizio Sarri, anayetakiwa Chelsea ataondoka. 

Siku chache zilizopita, Conte alinaswa na kamera za mapaparazi akiwa na Ancelotti katika mechi ya kumuaga mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo. 

Kwa muda mrefu sasa, Sarri amekuwa katika orodha ya makocha wanaotakiwa kwenda kukalia kiti cha Mwitalia mwenzake huyo. 

Hata hivyo, Chelsea wanatakiwa kujifikiria mara mbili juu ya mpango wao wa kuachana na Conte kwani watalazimika kumpa pauni milioni 9.6 kuvunja mkataba wake wa sasa.

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.